WATUMISHI SHAMBA LA MITI SAOHILL WAPEWA ELIMU YA SHERIA
Watumishi wa TFS - Shamba la Miti SaoHill wamepatiwa mafunzo mbalimbali ya sheria ikiwa ni sehemuya maadhimisho ya siku ya sheria nchini yanayoendeshwa na Mahakama ya Tanzania. Lengo la mafunzo haya ni kutoa elimu kuhusu sheria mbalimbali ambazo wanazitumia katika shughuli za kazi za kila siku.
Mafunzo hayo yameendeshwa kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU), Mahakama ya Tanzania, Uhamiaji, Maendeleo ya Jamii,Ardhi na Tume ya Usuluhishi na Migogoro ya kazi.Katika mafunzo hayo watumishi wametakiwa kuwa waadilifu katika utendaji wao wa kazi, kufuata haki katika kuhudumia wananchi bila kubagua na pia kushughulikia malalamiko ya wananchi kwa wakati.
Pichani: Meneja wa Shamba la Miti SaoHill Bw. Juma Mwita Msite akiongea wakati wa utoaji wa elimu ya sheria iliyoratibiwa na Mahakama Kuu ya Tanzania.
Pichani: Watumishi wa Shamba la Miti SaoHill wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa kuhusu sheria mbalimbali
No comments:
Post a Comment