Wadau wa Mazao ya
misitu waridhia uanzishwaji wa soko la pamoja
Wadau wa mazao ya misitu
katika shamba la miti Saohill wameridhia
uanzishwaji wa soko la pamoja la mazao ya misitu katika Shamba la Miti SaoHill katika
kikao kilichofanyika leo tarehe 13 Februari, 2020 katika ukumbi uliopo Shamba
la Miti SaoHill.
Kaimu Meneja wa shamba Bw.
Ignas Lupala amewaeleza wadau kuwa
serikali inaazimia kuanzishwa kwa soko la pamoja la mazao ya misitu ili kuwe na
eneo moja ambalo wanunuzi watapata mbao bora na kwa urahisi .
Amesema kuwa uanzishwaji wa
soko hili utasaidia wadau kuwa na uhakika wa kupata soko na wanunuzi kuwa na eneo la uhakika la kupata
bidhaa.
Naye Mwenyekiti wa wavunaji
Shamba la Miti SaoHill Bw. Christian Ahia amesema kuwa suala la soko limekuwa
ni chagamoto hivyo kwa uanzishwaji wa soko la pamoja utasaidia kuwaunganisha
wavunaji.
Hata hivyo wadau
wameipongeza serikali kupitia Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) kwa kuja na
mpango wa uanzishaji wa soko la pamoja na wameiomba serikali kuweka viwango vya mbao kwani hivi sasa kumekuwa na mbao ambazo ni changa
na hivyo kusababisa bei ya soko kuwa chini na hivyo kuwasababishia wao kupata
hasara.
Kikao hiki kimeitishwa
kufuatia maelekezo ya Naibu Kamisha Uhifadhi – Mipango na Masoko juu ya
uanzishwaji wa soko la pamoja ili iwe rahisi katika upatikana wa masoko wa
mazao ya misitu.
Pichani: Mwenyekiti wa Wavunaji shamba la Miti SaoHill Bw. Christian Ahia akizungumza wakati wa kikao cha kujadili juu ya uanzishwaji wa soko la pamoja la mzao ya misitu
Pichani: Kaimu Meneja wa Shamba la Miti SaoHill Bw. Ignas Lupala akizungumza na wadau wa mazao ya misitu wakati wa kikao cha kujadili juu ya uanzishwaji wa soko la pamoja la mazao ya misitu
Pichani Juu: Wadau wa mazao ya misitu katika Shamba la Miti SaoHill wakichangia mada wakati wa kikao cha kujadili juu ya uanzishwaji wa soko la pamoja la mazao ya misitu
No comments:
Post a Comment