Tuesday, June 14, 2016

TANGAZO KWA WADAU WALIO SHINDA MNADA

TANGAZO
Meneja wa Shamba la Miti Sao Hill kwa kushirikiana na Kamati ya Mnada Wa Miti uliofanyika makao makuu ya Shamba Ihefu, Mafinga Siku ya tarehe 07/06/2016 na tarehe 08/06/2016 anawatangazia wadau wote walioshinda katika mnada huo kwamba muda wa kulipia tozo za viunga walivyoshinda umeongezwa hadi siku ya Jumatano tarehe 15/06/2016.
Ikumbukwe mnada ulilenga kuongeza upatikanaji endelevu wa mazao ya misitu Sokoni pamoja na kukusanya mapato ya serikali hivyo ambaye alishinda katika mnada huo na akaacha kulipia tozo bila kutoa taarifa ya sababu ya kushindwa kufanya hivyo, atahesabika kama alikua na nia ya kuvuruga mnada huo na hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake ikiwa ni pamoja na kuingizwa kwenye orodha ya watu wasiostahili kufanya biashara yoyote kwenye ofisi za misitu na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania kwa ujumla.
MUHIMU:
KABLA YA KUKAMILISHA MALIPO NDUGU MTEJA UNATAKIWA KUFIKA OFISI YA UVUNAJI NA LESENI ILIYOPO MAKAO MAKUU YA SHAMBA LA MITI SAO HILL KUPATA KUTHIBITISHO WA UHALALI WA MALIPO KWENYE AKAUNTI YA SERIKALI.
ATAKAYESIKIA TANGAZO HILI AMTAARIFU MWENZAKE.
IMETOLEWA NA OFISI YA MENEJA WA SHAMBA LA MITI SAO HILL.
14/06/2016




Thursday, May 5, 2016

UANZISHAJI WA SHAMBA LA MITI









https://www.youtube.com/watch?v=AqZJP0ejrAc


https://www.youtube.com/watch?v=BcYW3mMep4w

Sunday, April 24, 2016

Monday, April 18, 2016

ZIFAHAMU SIFA ZA SHAMBA LA NYUKI



SIFA A SHAMBA LA NYUKI (MANZUKI)
I.             Kuwapo Kwa mimea inayotoa Maua yanayotoa chakula cha nyuki cha kutosha, Kwa mf. Sehemu yenye misitu, shamba la miti au mazao ya kilimo. Muda wa mimea kuchanua ujulikane kwa mfugaji nyuki ili aweze kupanga muda ambao atawezesha kundi la nyuki kujijenga na kukusanya mazao ya kutosha wakati mimea inapochanua Maua.

II.            Maji ya kutosha ni muhimu, nyuki huyatumia kupooza kupooza joto ndani ya mzinga, kulainisha chakula na kurekebisha utamu wa asali ambayo hulishwa majana.

III.           Mahali panapofikia ili kuwezesha usafirishaji wa vifaa na mazao ya nyuki nyakati za uvunaji.

IV.          Umbali wa kilomita tatu kutoka katika makazi ya watu,shule,hospitali na pasiwe mahali ambapo ni mapito ya mifugo. Inapolazimu kuwa na manzuki katika maeneo haya ,izungushiwe uzio wenye miti mirefu ili nyuki wanapokwenda nakurudi kutafuta cha kula wapiti juu
ili wasishambulie watu na wanyama. Umbali uliotajwa hapa ni kwa ajili ya nyuki  wanaouma tu.

V.            Mbali na maeneo ya kilimo kinachotumia kemikali kwa mfano kilimo cha tumbaku na korosho, manzuki yaanzishwe umbali wa  kilometa saba kutoka maeneo hayo. Hii ni kuzuia nyuki wasife kwa kemikali hizo, au kuzuia mizinga isiangushwe na pia kusababisha nyuki washindwe kurudi kwenye mizinga.

VI.          Kudhibiti uharibifu kutokana na maadui wa nyuki, wizi wa mizinga na mazao ya nyuki.

Viashiria Vifuatavyo hutumika sehemu mbalimbali kutambua muda wa kuvuna Asali..
i)Mwisho wa Msimu wa mvua na mwanzo wa Kangazi
ii)Maua au matunda ya mmea Fulani kupukutika
iii)Matunda ya mmea mwitu kutokeza
iv) Mazao ya shamabani kukomaa
v)Mngurumo wa nyuki wakusanyao chakula  kupungua
vi)Madume ya nyuki kuonekana yamekufa kwenye mlango ama chini ya mzinga
vii)Kundi la Nyuki kutanda nje ya Mzinga
viii)Gundi nyingi kuonekana katika mlango na matundu ya Mzinga
ix) Uzito wa Mzinga kuongezeka
x)Kijiti kuchomwa ndani ya Mzinga na kuona kama kina asali(Ukaguzi wa kienyeji)Njia hii haimuwezeshi mfugaji kujua kama asali imeiva ama mbichi.
xi)Sauti ya mzinga unapogongwa,inaashiria kama mzinga umejaa ama ni mtupu.
xii)Mwinamo wa mzinga kubadilika.

Nyuki iliaweze kuvutiwa na kuishi katika mzinga wako, nini wajibu wa Mfugaji?
Kwakuzingatia sifa za shamba la nyuki kama nilivyozieleza hapo juu,utakuwa umewawezesha nyuki kuishi bila kuhama katika Shamba lako la Nyuki/Manzuki,Aidha ,zipo njia za kienyeji na kitaalamu zinazoshauriwa kuwavutia Nyuki ndani ya Mzinga.Njia hiyo ni kupakaa NTA Kitaalamu kwenye mzinga wa Nyuki.

SHAMBA LA NYUKI LINAHITAJI WAFANYAKAZI WANGAPI?, AWE NA ELIMU GANI?
Shughuli ya Ufugaji wa Nyuki ni shughuli ambayo ni rahisi na haihitaji gharama kubwa, vibarua watahitajika sana kipindi cha mwanzo kwa ajili ya utundikwaji wa mizinga ambao wanatakiwa angalu miongoni pawe na watu wenye uzoefu wa kutundika mizinga kulingana na aina ya MANZUKI yako.Inashauriwa pia kuwa na mtaalamu kwa ajili ya ushauri mbalimbali hasa wakati wa kutundika mizinga na wakati wa uvunaji wa asali.Hivyo siyo lazima vibarua wawe na elimu kubwa ya Ufugaji wa nyuki.
MZINGA MMOJA WASTANI UNATOA LITA NGAPI ZA ASALI au KILO NGAPI?
Inategemea na sababu mbalimbali ,hata hivyo;kwa kawaida Mzinga mmoja unaweza kutoa lita 15- 20.Mzinga huo pia unaweza kutoa 25-30 KG.


IPI NI BEI YA ASALI KWA SASA?
Gharama ya Asali inategemea na maeneo tofauti tofauti kulingana na mazingira husika,hata hivyo bei kwa wastani kwa  sasa kwa Lita inaanzia 10-15 elfu.
Fursa ya Soko la nje pia ipo,tatizo ni consistency ya quantity na quality.
MASOKO YA ASALI YA TANZANIA YAPO WAPI? NINI MAHITAJI YA SOKO? BEI YA SOKO NI TSH NGAPI? KWA LITA AU KWA KILO?
Hili limekuwa swali la mara kwa mara kutoka kwa watu wenye nia ya ufugaji wa Nyuki,kweli ni kwamba bado kuna changamoto kuhusu soko la uhakika kwa ajili ya Asali,hata hivyo,bado kuna uwezekano wa kupata soko la ndani, sisi kama wadau wa Ufugaji Nyuki na Biashara ya Asali,tunalojukumu kubwa la kutoa hamasa kwa jamii yetu(Kazini i.e ofsini,shuleni,sehemu zetu za kupumzika,tunapowatembelea ndugu na jamaa zetu,sehemu za michezo n.k) ya kuwa,Asali ina umuhimu mkubwa kwa Afya ya Mwanadamu kutokana na uwezo wake wa kuwa na virutubisho na kuponya magonjwa mbalimbali,hivyo,kufanya Asali kuwa mojawapo ya chakula muhimu kila wakati wa mlo tupatapo chakula,tupatapo kifungua kinywa n.k,
Tuendelee kuielimisha jamii kuwa,matumizi ya Asali SI TU PINDI MTU APATAPO MATATIZO YA KIAFYA ,Bali wakati wote inafaa kutumia Asali.Kwa kufanya hivyo,jamii yetu itazingatia matumizi ya Asali na tutakuwa tumepanua soko la ndani la Asali. Vilevile,wazalishaji wa vitu vya kula kama Bakhresa kupitia bidhaa za Azam pamoja na ASAS DIARY n.k huko Iringa wamekuwa wanunuaji wa asali,hata hivyo, unaweza kuanzisha duka lako la asali hapo unapoishi au katika moja ya miji mikubwa kama Mwanza,Arusha,Mbeya na Dar es Salaam,unaweza pia kutafuta masoko kupitia MASOKO MAKUU YALIYOKO miji ya Dar es Salaa-kariakor,Mwanza,Mbeya,Tanga na Arusha,huko unaweza kubaliana na wauzaji wa masoko na kupata Soko la Asali.
Gharama ya sasa kwa Lita inaanzia 10-15 elfu. Fursa ya Soko la nje pia ipo,tatizo ni consistency ya quantity na quality.Tutaendelea kujadiliana zaidi kuhusu suala la Soko.
Neema Aminiufoo Lema,
Afisa misitu daraja la 2,
Email: nlema703@Gmail.com




Friday, April 15, 2016

ROYAL JELLY KATIKA SELI ZA MALKIA

Royal Jelly Katika Seli Ya Malkia

Royal Jelly ni secretion inayotolewa na nyuki wa asali na hutumika katika lishe ya mabuu, pamoja na Malkia wakubwa. Hutolea katika matezi (hypopharynx) ya nyuki vibarua, na kulishwa kwa mabuu wote katika koloni, bila kujali jinsia au tabaka.




UVUNAJI WA SELI ZA MALKIA

Uvunaji wa Seli za Malkia
Uvunaji wa Seli za Malkia