TANGAZO
Meneja wa
Shamba la Miti Sao Hill kwa kushirikiana na Kamati ya Mnada Wa Miti uliofanyika
makao makuu ya Shamba Ihefu, Mafinga Siku ya tarehe 07/06/2016 na tarehe
08/06/2016 anawatangazia wadau wote walioshinda katika mnada huo kwamba muda wa
kulipia tozo za viunga walivyoshinda umeongezwa hadi siku ya Jumatano tarehe
15/06/2016.
Ikumbukwe
mnada ulilenga kuongeza upatikanaji endelevu wa mazao ya misitu Sokoni pamoja
na kukusanya mapato ya serikali hivyo ambaye alishinda katika mnada huo na
akaacha kulipia tozo bila kutoa taarifa ya sababu ya kushindwa kufanya hivyo,
atahesabika kama alikua na nia ya kuvuruga mnada huo na hatua za kisheria
zitachukuliwa dhidi yake ikiwa ni pamoja na kuingizwa kwenye orodha ya watu
wasiostahili kufanya biashara yoyote kwenye ofisi za misitu na Wakala wa Huduma
za Misitu Tanzania kwa ujumla.
MUHIMU:
KABLA YA
KUKAMILISHA MALIPO NDUGU MTEJA UNATAKIWA KUFIKA OFISI YA UVUNAJI NA LESENI
ILIYOPO MAKAO MAKUU YA SHAMBA LA MITI SAO HILL KUPATA KUTHIBITISHO WA UHALALI
WA MALIPO KWENYE AKAUNTI YA SERIKALI.
ATAKAYESIKIA TANGAZO HILI AMTAARIFU
MWENZAKE.
IMETOLEWA NA OFISI YA
MENEJA WA SHAMBA LA MITI SAO HILL.
14/06/2016
Slot88 Casino Bonus Code: $10 FREE + $25 Free Chip
ReplyDeleteSlot88 Casino Bonus Code is NEWSRBONUSSEEKER. Check out the latest 거제 출장안마 online 서울특별 출장마사지 casino bonus 아산 출장안마 codes 여주 출장마사지 from this fantastic 인천광역 출장마사지 provider:.