SIFA A SHAMBA LA NYUKI (MANZUKI)
I. Kuwapo
Kwa mimea inayotoa Maua yanayotoa chakula cha nyuki cha kutosha, Kwa mf. Sehemu
yenye misitu, shamba la miti au mazao ya kilimo. Muda wa mimea kuchanua
ujulikane kwa mfugaji nyuki ili aweze kupanga muda ambao atawezesha kundi la
nyuki kujijenga na kukusanya mazao ya kutosha wakati mimea inapochanua Maua.
II. Maji ya
kutosha ni muhimu, nyuki huyatumia kupooza kupooza joto ndani ya mzinga,
kulainisha chakula na kurekebisha utamu wa asali ambayo hulishwa majana.
III. Mahali
panapofikia ili kuwezesha usafirishaji wa vifaa na mazao ya nyuki nyakati za
uvunaji.
IV. Umbali wa
kilomita tatu kutoka katika makazi ya watu,shule,hospitali na pasiwe mahali
ambapo ni mapito ya mifugo. Inapolazimu kuwa na manzuki katika maeneo haya
,izungushiwe uzio wenye miti mirefu ili nyuki wanapokwenda nakurudi kutafuta
cha kula wapiti juu
ili wasishambulie watu na wanyama. Umbali uliotajwa hapa ni
kwa ajili ya nyuki wanaouma tu.
V. Mbali na
maeneo ya kilimo kinachotumia kemikali kwa mfano kilimo cha tumbaku na korosho,
manzuki yaanzishwe umbali wa kilometa
saba kutoka maeneo hayo. Hii ni kuzuia nyuki wasife kwa kemikali hizo, au
kuzuia mizinga isiangushwe na pia kusababisha nyuki washindwe kurudi kwenye
mizinga.
VI. Kudhibiti
uharibifu kutokana na maadui wa nyuki, wizi wa mizinga na mazao ya nyuki.
Viashiria Vifuatavyo hutumika sehemu mbalimbali kutambua
muda wa kuvuna Asali..
i)Mwisho wa Msimu wa mvua na mwanzo wa Kangazi
ii)Maua au matunda ya mmea Fulani kupukutika
iii)Matunda ya mmea mwitu kutokeza
iv) Mazao ya shamabani kukomaa
v)Mngurumo wa nyuki wakusanyao chakula kupungua
vi)Madume ya nyuki kuonekana yamekufa kwenye mlango ama
chini ya mzinga
vii)Kundi la Nyuki kutanda nje ya Mzinga
viii)Gundi nyingi kuonekana katika mlango na matundu ya
Mzinga
ix) Uzito wa Mzinga kuongezeka
x)Kijiti kuchomwa ndani ya Mzinga na kuona kama kina
asali(Ukaguzi wa kienyeji)Njia hii haimuwezeshi mfugaji kujua kama asali imeiva
ama mbichi.
xi)Sauti ya mzinga unapogongwa,inaashiria kama mzinga umejaa
ama ni mtupu.
xii)Mwinamo wa mzinga kubadilika.
Nyuki iliaweze kuvutiwa na kuishi katika mzinga wako, nini
wajibu wa Mfugaji?
Kwakuzingatia sifa za shamba la nyuki kama nilivyozieleza
hapo juu,utakuwa umewawezesha nyuki kuishi bila kuhama katika Shamba lako la
Nyuki/Manzuki,Aidha ,zipo njia za kienyeji na kitaalamu zinazoshauriwa
kuwavutia Nyuki ndani ya Mzinga.Njia hiyo ni kupakaa NTA Kitaalamu kwenye
mzinga wa Nyuki.
SHAMBA LA NYUKI LINAHITAJI WAFANYAKAZI WANGAPI?, AWE NA
ELIMU GANI?
Shughuli ya Ufugaji wa Nyuki ni shughuli ambayo ni rahisi na
haihitaji gharama kubwa, vibarua watahitajika sana kipindi cha mwanzo kwa ajili
ya utundikwaji wa mizinga ambao wanatakiwa angalu miongoni pawe na watu wenye
uzoefu wa kutundika mizinga kulingana na aina ya MANZUKI yako.Inashauriwa pia
kuwa na mtaalamu kwa ajili ya ushauri mbalimbali hasa wakati wa kutundika
mizinga na wakati wa uvunaji wa asali.Hivyo siyo lazima vibarua wawe na elimu
kubwa ya Ufugaji wa nyuki.
MZINGA MMOJA WASTANI UNATOA LITA NGAPI ZA ASALI au KILO
NGAPI?
Inategemea na sababu mbalimbali ,hata hivyo;kwa kawaida
Mzinga mmoja unaweza kutoa lita 15- 20.Mzinga huo pia unaweza kutoa 25-30 KG.
IPI NI BEI YA ASALI KWA SASA?
Gharama ya Asali inategemea na maeneo tofauti tofauti
kulingana na mazingira husika,hata hivyo bei kwa wastani kwa sasa kwa Lita inaanzia 10-15 elfu.
Fursa ya Soko la nje pia ipo,tatizo ni consistency ya
quantity na quality.
MASOKO YA ASALI YA TANZANIA YAPO WAPI? NINI MAHITAJI YA
SOKO? BEI YA SOKO NI TSH NGAPI? KWA LITA AU KWA KILO?
Hili limekuwa swali la mara kwa mara kutoka kwa watu wenye
nia ya ufugaji wa Nyuki,kweli ni kwamba bado kuna changamoto kuhusu soko la
uhakika kwa ajili ya Asali,hata hivyo,bado kuna uwezekano wa kupata soko la
ndani, sisi kama wadau wa Ufugaji Nyuki na Biashara ya Asali,tunalojukumu kubwa
la kutoa hamasa kwa jamii yetu(Kazini i.e ofsini,shuleni,sehemu zetu za
kupumzika,tunapowatembelea ndugu na jamaa zetu,sehemu za michezo n.k) ya
kuwa,Asali ina umuhimu mkubwa kwa Afya ya Mwanadamu kutokana na uwezo wake wa
kuwa na virutubisho na kuponya magonjwa mbalimbali,hivyo,kufanya Asali kuwa
mojawapo ya chakula muhimu kila wakati wa mlo tupatapo chakula,tupatapo
kifungua kinywa n.k,
Tuendelee kuielimisha jamii kuwa,matumizi ya Asali SI TU
PINDI MTU APATAPO MATATIZO YA KIAFYA ,Bali wakati wote inafaa kutumia Asali.Kwa
kufanya hivyo,jamii yetu itazingatia matumizi ya Asali na tutakuwa tumepanua
soko la ndani la Asali. Vilevile,wazalishaji wa vitu vya kula kama Bakhresa
kupitia bidhaa za Azam pamoja na ASAS DIARY n.k huko Iringa wamekuwa wanunuaji
wa asali,hata hivyo, unaweza kuanzisha duka lako la asali hapo unapoishi au
katika moja ya miji mikubwa kama Mwanza,Arusha,Mbeya na Dar es Salaam,unaweza
pia kutafuta masoko kupitia MASOKO MAKUU YALIYOKO miji ya Dar es
Salaa-kariakor,Mwanza,Mbeya,Tanga na Arusha,huko unaweza kubaliana na wauzaji
wa masoko na kupata Soko la Asali.
Gharama ya sasa kwa Lita inaanzia 10-15 elfu. Fursa ya Soko
la nje pia ipo,tatizo ni consistency ya quantity na quality.Tutaendelea
kujadiliana zaidi kuhusu suala la Soko.
Neema Aminiufoo Lema,
Afisa misitu daraja
la 2,
Email:
nlema703@Gmail.com
Inapendeza
ReplyDeleteNaomba kupata nafasi ya kufanya ziara ya kimafunzo kwenye shamba la nyuki. Mimi ni mfugaji nyuki mpya baada ya kustaafu utumishi wa umma
ReplyDeleteNyuki wadogo wanazalisha asali kiasi gani, je naweza kuwafuga nymbani kwenye makazi ya watu
ReplyDelete